Tuesday, August 9, 2011

Anthony Luvanda na kazi yake nzuri ya U-MC

Kwa wengine ni mara ya kwanza kulisikia jina hili. Kwa wengine jina hili si geni sana. Anthony Luvanda ni mtangazaji, mshereheshaji (MC), na mfanyakazi wa benki moja maarufu jijini Dar es Salaam. Hayo ni machache katika mengi usiyoyafahamu kuhusu kijana huyu mtanashati na aliyejaliwa vipaji lukuki na mwenyezi Mungu.

Kijana huyu ana majukumu mengi binafsi pamoja na majukumu mengine ya kijamii. Lakini leo ninataka kukudokeza kidogo tu kuhusu jukumu au kazi moja tu ambayo Anthony Luvanda amekuwa akiifanya kwa muda sasa na inayoonekana kumkaa kama vile alizaliwa nayo. Kazi hii si nyingine bali ni ya ushereheshaji, maarufu kama u-MC. Kwa lugha ya kiingereza ikijulikana zaidi kama ‘Master of Ceremony’.

Anthony Luvanda ambaye nimebahatika kusoma naye katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kufanya naye kazi katika sehemu mbili na nyakati mbili tofauti, kwa kweli ni mahiri sana katika kazi hii kiasi kwamba unaweza ukadhani amesomea mahali fulani.

Kutokana na umuhimu wa suala hili ambalo kwake ni kazi ama biashara, na kutokana na blog yangu kuwa inayohusu mambo ya shughuli za kibiashara, basi ni muhimu nikalielezea kwa marefu yake na mapana yake ili ninyi wasomaji wangu muweze kuelewa vizuri zaidi.

Hivyo basi kwa leo naomba niishie hapa, nikiwaacha na picha ya kijana huyu mahiri akiwa katika mojawapo ya shughuli zake katika moja ya matukio muhimu nchini.


 

Nitarejea kwenu muda si mrefu na mambo matamu na mazuri zaidi kuhusu shughuli hii na hususan kuhusu kijana huyu, Anthony Luvanda.

Asanteni sana.

Andrea Muhozya.

No comments:

Post a Comment