Friday, August 12, 2011

Je Wajua kuwa machungwa ni zao la matunda linalovunwa sana duniani?

CHUNGWA ni tunda la msimu. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Jina la kisayansi ni Citrus aurantium L. var. sinensis L. au Citrus sinensis (L.) Osbeck.

Tunda lenyewe ni kijani na rangi inabadilika kuelekea njano likiiva. Pamoja na limau, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa. Siku hizi ni tunda linalovunwa zaidi kati ya matunda chungwa.

Asili yake ni katika Asia ya Kusini-Mashariki ambako lilioteshwa na wakulima. Kuna aina mbili yanayotofautiana kwa ladha ama chungu au tamu. Lenye ladha chungu liliwahi kusambaa duniani hivyo jina la Kiswahili limetunza ladha hii hata kama matunda mengi yanayopandwa siku hizi ni aina tamu.

Chungwa tamu lilisambaa kote duniani baada ya Wareno kuchukua machipuko yake na kuyapanda kwanza Ureno baadaye hata Amerika na Afrika kuanzia karne ya 15. Chungwa, na hasa chungwa tamu, ni jamii ya matunda ya citrus, na huaminika kuwa yalikuzwa miongoni mwa enzi za pomelo na tangerine.

Mti wake mdogo utoao maua hufikia urefu takribani mita kumi na majani yake yasiyokauka muda wote. Machungwa asili yake ni huko kusini mwa Asia. Tunda lifahamikalo kisayansi kama citrus sinesis huitwa chungwa tamu ili kutofautisha na citrus aurantium, chungwa chungu.

Matunda yote jamii ya jenasi ya citrus, huzaliana na familia yao hujumuisha machungwa, ndimu na limao. Matunda ya jamii hii huonwa kama ni ya aina ya beri sababu ya kuwa na mbegu nyingi, kuwa laini na nyama nyingi huku yakikua kutoka kwenye ovari moja.

Kama ilivyo kwa jamii ya matunda ya citrus, machungwa nayo huwa na hali ya asidi, yenye kiwango cha pH karibu na 2.5 -3, kulingana na umri wake, ukubwa na aina ya chungwa. Japo si kama ilivyo kwa limao, bado machungwa huwa na kiwango cha asidi cha kutosha, sawa kabisa na hata siki ya nyumbani.

Machungwa kwa kawaida hulimwa kwa ajili ya biashara na hulimwa maeneo mengi duniani. Wazalishaji wa machungwa wanaoongoza duniani ni Brazili, Marekani na Meksiko. Machungwa huathirika kwa haraka sana na ukungu hivyo huhitaji matunzo mazuri pindi joto dogo sana linapotegemewa.

Michungwa huweza kukuzwa maeneo yenye joto na hata yale yenye baridi. Kama ilivyo kwa matunda mengine ya citrus, ili kupata mazao mazuri haina budi kukuza michungwa katika joto la nyuzijoto 15.5 °C - 29 °C.

Miti ya machungwa iliooteshwa kutokana na mbegu zilizonunuliwa madukani inaweza kuwa tofauti kabisa na ile miti ya asili iliyozalisha mbegu hizo. Hii hutokana na mabadiliko ya kizazi yanayotokana na kuchanganywa mbegu kisayansi kwa muda mrefu.

Ili kupata mmea wa mchungwa kama tunda ambalo linanunuliwa, huna budi kuitunza mbegu hiyo kwenye unyevunyevu kisha tu baada ya kuzitua kwenye tunda na kuziotesha katika hali ya unyevu; na pindi mmea uchipuapo hapo ukapandwe kwenye udongo kusudiwa.

Machungwa yanakuzwa katika hali mbalimbali za joto duniani kote, na ladha yake hubadilika kuanzia hali ya utamu mpaka uchungu kabisa. Tunda kwa kawaida humenywa na kuliwa au huminywa na sharubati yake kunywewa.

Limezungukwa na ganda lenye ladha chungu lakini huweza kukamuliwa na kuondolewa maji yake na kutumika kwa chakula cha mifugo. Pia, hutumika kuongeza ladha ya vyakula vingine na hata maganda yake hufaa kwa kazi hii.

Sehemu nyeupe ya ndani, kati ya nyama na ganda la nje nayo huwa na vitamini sawa kabisa na nyama ya ndani. Sharubati ya machungwa ndiyo bidhaa kuu kuliko zote ya machungwa. Huweza kuzalishwa kwa matumizi ya nyumbani lakini hasa hufanywa kwa minajili ya biashara.

Sharubati ya kugandishwa ya machungwa hutengenezwa kutokana na majimaji ya machungwa pia. Mafuta ya machungwa ni bidhaa ndogo inayotengenezwa kwa kukamua maganda ya machungwa. Hutumika kwa kuongeza ladha ya chakula na zaidi kwenye utengenezaji wa manukato.

Maua ya machungwa nayo hupendwa kwa harufu yake nzuri na hutumika mara nyingi nyakati za harusi na huhusishwa na bahati njema. Majani ya michungwa yanaweza kutumika kutengenezea chai.

Licha ya kwamba zao hili hufahamika duniani kutokana na mahitaji yake, lakini bado halijapewa kipaumbele nchini hasa kutokana na wakulima kutokuwa na uhakika wa soko kwa ajili ya bidhaa zao.

Serikali inahitajika kuwafikiria na kuwapa mbinu za kuweza kuboresha kilimo chao ili waweze kuvuna matunda mengi yanayohitajika. Ni wazi kwamba kuna wakulima wachache ambao wamepata fursa ya kufanya kazi na kampuni mbalimbali ambazo hutengeneza bidhaa za matunda, hao ndio wanaonufaika.

Lakini pia wapo ambao wana moyo ya kulima machungwa kwa wingi lakini wanaendelea kukandamizwa na wafanyabiashara wakubwa ambao huwanunuza katika mashamba. Wakulima wengi hawana vikundi vya ushirika kwani wengi hufanya kazi kwa kujitegemea.

Hiyo ni changamoto kubwa inayomfanya aendelee kukandamizwa na mfanyabiashara mkubwa. Wangekuwa na vikundi ni wazi kwamba hata bei wangejipangia wenyewe na wangekuwa na uwezo wa kusafirisha sokoni na kuuzwa kwa bei wanayotaka.

Machungwa huoza haraka. Wakati mwingine wakulima wanapata hasara kubwa hasa pale ambapo wanasubiri usafiri wa kupeleka bidhaa zao sokoni, kuna maeneo mengine barabara sio nzuri, hivyo mpaka yafike sokoni mengi yanakuwa yameoza.

Bado hawana uelewa wa kutosha ni kwa jinsi watahifadhi matunda yao yasiweze kuharibika mapema. Hiyo ni changamoto kubwa inayowakumba wakulima na wafanyabiashara wa machungwa. Kwani baadhi yao wamekuwa wakihifadhi ilimradi wanavyojua wao.

Pia, wafanyabiashara na wakulima wa machungwa hupenda kurundikana sehemu moja wakati wa msimu wa machungwa hivyo pia, biashara kuwa ngumu kwa vile wanauza kiushindani. Zipo sehemu nyingi ambazo wanaweza kufanya biashara zao na zikatoka.

Hufahamika kuwa, siku zote mazao ya mboga na matunda yana thamani kubwa kuliko mazao mengine na yanahitaji uangalifu mkubwa zaidi wakati wa uzalishaji. Udhibiti wa visumbufu vya mazao hayo wakati yakiwa shambani ni muhimu ufanyike kwa wakati unaotakiwa na kwa ufanisi ili kuleta matokeo mazuri katika uzalishaji.

Mazao ya matunda yaliyo machache na hafifu kutokana na uzalishaji duni huwa na faida ndogo ambayo inakatisha tama katika kuwekeza wakati wa kutumia teknolojia za utunzaji bora na usindikaji na hifadhi.

Ili kupata mazao bora na kupunguza uharibifu, mkulima hana budi kuzingatia kanuni za kilimo bora cha matunda pamoja na mbinu bora za uvunaji, utayarishaji na uhifadhi. Mbinu hizi zinahusisha pia usindikaji wa mazao hayo wenye lengo la kuongeza ubora na kuhifadhi kwa muda mrefu kwa ajili ya masoko na kuwezesha upatikanaji wakati wote.

(Makala kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Habari Leo Agosti 2, 2011)

Wednesday, August 10, 2011

BIASHARA YAKO NI NINI? Utalijibuje swali hili?

BIASHARA YAKO NI NINI?

Unaweza ukajibu swali hili kwa kuangalia vitu viafutavyo nini unazalish na kwa ajili ya nani?
Maana yake ni kuwa biashara ina mambo mawili
Uzalishaji (Production)
Masoko (Marketing)
Kitu cha msingi kukumbuka uko katika biashara ili kuzalisha /kutafuta pesa.
Maana yake ni kuwa lazima uwe na vitu vya kuuza na pia lazima uwe na watu wa kununua hivyo vitu vyako(kwa maana nyingine ni lazima uwe na bidhaa/huduma na pia wawepo wanunuzi wa bidhaa zako.)
Kupata vitu unavyotaka kuuza unahitaji uzalishaji (bidhaa/huduma) na pia kutafuta masoko ya kuuzia hizo bidhaa/huduma ulizozalisha.
Kwa hiyo biashara kwa maana nyingine ni bidhaa/huduma na masoko.
Tuanze na uzalishaji (Production)
Mfano fikiria
Kama wewe ni mtengenezaji wa viatu/miwani ya jua, ukiulizwa biashara yoko ni nini , utasema ni kutengeneza miwani /viatu.lakini hii ni biashara yako kweli?
Unachotengeneza ndicho unachauza?
Kama unatengeneza miwani ya jua ,kutengeneza miwani ya jua sio njia pekee ya kuelezea uzalishaji wako.
Biashara yako ungeweza kuielezea kuwa ni kuzuia macho kupigwa na mionzi ya jua.
Kama utasema “nina biashara ya kutengeneza miwani ya jua” ni lazima utambue
Kuwa miwani ina vipande viwili vya plastiki vya rangi vilivyoshikwa na fremu za
Plastiki kwenye uso wako.
Hakuna mtu atakeye nunua miwani kwa kuwa anataka viande viwili vya plastiki/glasi vya rangi aviweke usoni mwake.
(HAPA NI LAZIMA UZALISHE ZAIDI YA MIWANI.)
Unapoelezea biashara yako lazima pia uelezee kuhusu masoko yake
(It’s marketing) mfano ;ukisema biashara yako ni kuuza miwani kwa waitali.
Kumbuka biashara ni uzalishaji na masoko.
Tuzumgumzie masoko (marketing)
“Utasema biashara yako ni biashara ya kutengeneza miwani za jua kwa waitalia”
Hii ni nzuri kidogo lakini kuna mamilioni ya waitalia , hakika huko katika biashara ya kuwatengenezea miwani za jua mamilioni ya waitali wote.
Fikiri biashara yako katika hali ya kwanini hawa watu wananunua miwani za jua?
Hapa biashara yako itakuwa “kutengeneza miwani ya jua ambayo inazuia mionzi kwa ajili ya waitalia wanopenda usalama wa macho yao"
Mfano ukisema biashara yako ni kuzalisha fulana za kampuni ya ukwamba ;
Ukwamba akakupatia kila kitu (malighafi zote ) kwa ajili ya uzalishaji na aina ya fulana ,mfano na ukubwa wa hizo fulana. Hapa maana yake ni kwamba ukwamba anahitaji uweke gharama za uzalishaji tu hasa wafanya kazi (labour costs)
Je unafikiri biashara yako ni nini?
Je kampuni ya ukwamba kiuhakika inanunua nini hasa kutoka kwako?
Je ni bei rahisi ya ufanyajikazi wako?(low cost of your labour).


Muhimu;
Kama hutasimamia vizuri bishara yako/kampuni yako au utachelewesha mzigo, mzigo ukawa chini ya kiwango,ukubwa tofauti, rangi tofauti na mlivyokubaliana, Ukwamba hata nunua huduma toka kwako hata kama una bei rahiasi kuliko kampuni yoyote hapa duniani.
Kutokana na maelezo hayo unaweza kusema biashara yako ni kutoa huduma (services) kuliko kutengeneza bidhaa.
Japokua unampatia ukwamba bidhaa za fulana,lakini ukwamba anapenda au anavutiwa na huduma yako ya usimamizi wa uzalishaji.
Biashara yako hapa ni kuuza utaalam wako wa usimamizi wa uzalishaji kwa kampuni ya ukwamba.(selling production management skills)
“Unachozalisha kinaweza kuwa sicho unachokiuza”


Ili kufafanua vizuri kuhusu mada hiyo hapo juu hebu jaribu kufikiria kuhusu magazeti
Magazeti yanauza nini?
Unaweza kufikiri na kusema kuwa magezeti yanauza habari kwa jamii,
Lakini jiulize mwenyewe kuuza magazeti kutaweza kuzalisha hela za kutosho kuendesh kampuni? Hela itakayopatikana haitoshi, kwani kuchapisha nakala moja
bei yake ni mara mbili ya bei ya kuuzia gazeti.
Hapa makampuni ya magazetai yanauza nafasi za matangazo.
Na ndio chanzo kikibwa cha mapato yao.
(They produce what they don’t sale and they sale what they don’t produce)


Muhimu;
Kama utashindwa kujua hasa kampuni yako iko katika biashara gani /inauza nini/
Inazalisha nini utakuwa umepoteza mwelekeo na hutatengeneza faida ambayo ndio msingi wa kuwa katika biashara (money making)


Hitimisho
1. unachozalisha/unachotengeneza kinaweza kuwa sicho unachouza.
Kujua uko katika biashara gani au nini biashara yako lazima ufikirie haya;
Kwa nini wananunua toka kwako?
2. wakati unafikiria kuhusu nani watanunua kutoka kwako ,fikiria pia kuhusu nani anahusika katika mafanikio yako ya kifedha ya kampuni
Watanzania wengi hatujui hasa ni nini biashara zetu(what is the business of your enterprise) hii inasababisha watu wengi sana kupata hasara na kufunga baadhi ya makampuni yao.

Ahsanteni sana
Karibuni wadau wote kwa maoni na ushauri.
source www.jamiiforums.com

Biashara Yako Ni Nini?

BIASHARA YAKO NI NINI?

Unaweza ukajibu swali hili kwa kuangalia vitu viafutavyo nini unazalish na kwa ajili ya nani?
Maana yake ni kuwa biashara ina mambo mawili
Uzalishaji (Production)
Masoko (Marketing)
Kitu cha msingi kukumbuka uko katika biashara ili kuzalisha /kutafuta pesa.
Maana yake ni kuwa lazima uwe na vitu vya kuuza na pia lazima uwe na watu wa kununua hivyo vitu vyako(kwa maana nyingine ni lazima uwe na bidhaa/huduma na pia wawepo wanunuzi wa bidhaa zako.)
Kupata vitu unavyotaka kuuza unahitaji uzalishaji (bidhaa/huduma) na pia kutafuta masoko ya kuuzia hizo bidhaa/huduma ulizozalisha.
Kwa hiyo biashara kwa maana nyingine ni bidhaa/huduma na masoko.
Tuanze na uzalishaji (Production)
Mfano fikiria
Kama wewe ni mtengenezaji wa viatu/miwani ya jua, ukiulizwa biashara yoko ni nini , utasema ni kutengeneza miwani /viatu.lakini hii ni biashara yako kweli?
Unachotengeneza ndicho unachauza?
Kama unatengeneza miwani ya jua ,kutengeneza miwani ya jua sio njia pekee ya kuelezea uzalishaji wako.
Biashara yako ungeweza kuielezea kuwa ni kuzuia macho kupigwa na mionzi ya jua.
Kama utasema “nina biashara ya kutengeneza miwani ya jua” ni lazima utambue
Kuwa miwani ina vipande viwili vya plastiki vya rangi vilivyoshikwa na fremu za
Plastiki kwenye uso wako.
Hakuna mtu atakeye nunua miwani kwa kuwa anataka viande viwili vya plastiki/glasi vya rangi aviweke usoni mwake.
(HAPA NI LAZIMA UZALISHE ZAIDI YA MIWANI.)
Unapoelezea biashara yako lazima pia uelezee kuhusu masoko yake
(It’s marketing) mfano ;ukisema biashara yako ni kuuza miwani kwa waitali.
Kumbuka biashara ni uzalishaji na masoko.
Tuzumgumzie masoko (marketing)
“Utasema biashara yako ni biashara ya kutengeneza miwani za jua kwa waitalia”
Hii ni nzuri kidogo lakini kuna mamilioni ya waitalia , hakika huko katika biashara ya kuwatengenezea miwani za jua mamilioni ya waitali wote.
Fikiri biashara yako katika hali ya kwanini hawa watu wananunua miwani za jua?
Hapa biashara yako itakuwa “kutengeneza miwani ya jua ambayo inazuia mionzi kwa ajili ya waitalia wanopenda usalama wa macho yao"
Mfano ukisema biashara yako ni kuzalisha fulana za kampuni ya ukwamba ;
Ukwamba akakupatia kila kitu (malighafi zote ) kwa ajili ya uzalishaji na aina ya fulana ,mfano na ukubwa wa hizo fulana. Hapa maana yake ni kwamba ukwamba anahitaji uweke gharama za uzalishaji tu hasa wafanya kazi (labour costs)
Je unafikiri biashara yako ni nini?
Je kampuni ya ukwamba kiuhakika inanunua nini hasa kutoka kwako?
Je ni bei rahisi ya ufanyajikazi wako?(low cost of your labour).


Muhimu;
Kama hutasimamia vizuri bishara yako/kampuni yako au utachelewesha mzigo, mzigo ukawa chini ya kiwango,ukubwa tofauti, rangi tofauti na mlivyokubaliana, Ukwamba hata nunua huduma toka kwako hata kama una bei rahiasi kuliko kampuni yoyote hapa duniani.
Kutokana na maelezo hayo unaweza kusema biashara yako ni kutoa huduma (services) kuliko kutengeneza bidhaa.
Japokua unampatia ukwamba bidhaa za fulana,lakini ukwamba anapenda au anavutiwa na huduma yako ya usimamizi wa uzalishaji.
Biashara yako hapa ni kuuza utaalam wako wa usimamizi wa uzalishaji kwa kampuni ya ukwamba.(selling production management skills)
“Unachozalisha kinaweza kuwa sicho unachokiuza”


Ili kufafanua vizuri kuhusu mada hiyo hapo juu hebu jaribu kufikiria kuhusu magazeti
Magazeti yanauza nini?
Unaweza kufikiri na kusema kuwa magezeti yanauza habari kwa jamii,
Lakini jiulize mwenyewe kuuza magazeti kutaweza kuzalisha hela za kutosho kuendesh kampuni? Hela itakayopatikana haitoshi, kwani kuchapisha nakala moja
bei yake ni mara mbili ya bei ya kuuzia gazeti.
Hapa makampuni ya magazetai yanauza nafasi za matangazo.
Na ndio chanzo kikibwa cha mapato yao.
(They produce what they don’t sale and they sale what they don’t produce)


Muhimu;
Kama utashindwa kujua hasa kampuni yako iko katika biashara gani /inauza nini/
Inazalisha nini utakuwa umepoteza mwelekeo na hutatengeneza faida ambayo ndio msingi wa kuwa katika biashara (money making)


Hitimisho
1. unachozalisha/unachotengeneza kinaweza kuwa sicho unachouza.
Kujua uko katika biashara gani au nini biashara yako lazima ufikirie haya;
Kwa nini wananunua toka kwako?
2. wakati unafikiria kuhusu nani watanunua kutoka kwako ,fikiria pia kuhusu nani anahusika katika mafanikio yako ya kifedha ya kampuni
Watanzania wengi hatujui hasa ni nini biashara zetu(what is the business of your enterprise) hii inasababisha watu wengi sana kupata hasara na kufunga baadhi ya makampuni yao.
ahsante sana
karibuni wadau wote kwa maoni na ushuri.

source www.jamiiforums.com

Wese kama kawa: Wafanyabiashara ya Mafuta Wasalimu Amri.

Wafanyabiashara ya mafuta wasalimu amri  
Wednesday, 10 August 2011 23:47


KAMPUNI nne zilizopewa amri na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), ya kurejesha huduma hiyo mara moja za BP, Oilcom, Engen na Camel Oil zimesalimu amri na kuanza usambazaji na uuzaji wa mafuta katika vituo mbalimbali nchini.Hata hivyo, katika baadhi ya vituo jijini Dares Salaam, utoaji wa huduma hiyo ulikuwa kusuasua hali iliyowafanya baadhi ya vijana kufunga barabara na kuvizingira wakitaka kuhudumiwa kwa nguvu.Mbali ya kufunga barabara na kuzingira vituo, vijana hao pia walikuwa wakiandamana barabarani kuelekea kituo kimoja baada ya kingine hasa vile vilivyopo kando kando ya Barabara ya Mandela.

Polisi waingia vituoniPolisi jana walikuwa wakifuatilia kwa karibu usalama katika vituo vya kuuzia mafuta kwa askari wake kufanya doria vituoni.Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kutokana na kauli ya Serikali, jeshi hilo limelazimika kulinda usalama na kukagua kuona ni vituo vilivyokuwa vikitii agizo hilo na vile vilivyokaidi.

“Hili suala linahitaji usimamizi wa hali ya juu, unajua tumelazimika kulinda usalama kwa wananchi kutokana na hizo foleni. Pia tunavikagua kujua kama vinatoa huduma,” alisema.

Camel wakutana lakini wauza mafuta
Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Camel ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alisema wameanza kutekeleza amri hiyo na tayari malori yalianza kuchukua mafuta na kusambaza katika vituo.

Alisema kazi hiyo ilianza jana mapema asubuhi na kwamba sambamba na hilo, viongozi wa ngazi za juu walikuwa kwenye mkutano wa ndani kujadili namna ya utekelezaji wa agizo hilo.Waandishi wa gazeti hili walifika kwenye hifadhi ya kampuni hiyo, Kurasini na kushuhudia malori makubwa yakipakia shehena ya mafuta kupeleka vituoni.

Engen yajikosha kwa Serikali
Engen, baada ya Mkurugenzi wake, Selan Naidoo kutuhumiwa kuidharau Serikali kwa kuipa saa 24 ifidie hasara itakayopata kutokana na bei mpya elekezi, jana imeibuka na kusema kwamba imekuwa na uhusiano mzuri na Serikali ya Tanzania na wakati wote imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Wayne Hartmann wakati wote kampuni hiyo imekuwa na malengo chanya kwa Tanzania na kwamba msimamo utakuwa wa kudumu kwao kwa wakati wote watakaokuwa wakiendesha biashara ya mafuta nchini.

Alisema kauli iliyotolewa na Naidoo kuhusu bei mpya za mafuta zilizotangazwa na Serikali kuwa ni msimamo wa kampuni hiyo na haihusiani kwa namna yoyote na kampuni nyingine za mafuta nchini.

Hata hivyo, Hartmann alisema kuwa bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika mwanzoni mwa mwezi huu, zimeyaweka makampuni ya mafuta katika wakati mgumu na mengi yamejikuta yakiuza kwa bei ya hasara.

Kwa upande wake Naidoo alisema vituo vingi vinavyomilikiwa na kampuni hiyo vingeanza kutoa huduma hiyo muda wowote kuanzia jioni kwa kuwa nyakati za mchana baadhi havikuweza kutoa huduma hiyo kwa kuwa havikuwa na mafuta.


Oilcom: Tumetekeleza maagizo
Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo ya Oilcom, Ahmed Bathawab alisema jana kwamba wametii agizo la Serikali na kusambaza mafuta kwenye vituo vyote vilivyopo chini ya kampuni hiyo.Alisema kampuni hiyo inasambaza mafuta kwa vituo zaidi ya 70 nchini kote, huku baadhi yake vikimilikiwa na kampuni hiyo na nyingine zikiwa chini ya washirika wake wa biashara.

Kuhusu agizo la kujieleza alisema wamepatiwa fomu na kujaza kisha kuzirudisha serikalini.“Tumetekeleza agizo la Serikali pamoja na masharti yake. Tumefungua vituo vyetu vya mafuta na kuhusu kujieleza walituletea fomu, tumejaza na kurudisha,” alisema Bathawab.Alisema kampuni yake imefungua vituo vyake 16 vya jijini Dar es Salaam na zaidi ya 70 vilivyopo nchi nzima na kueleza kwamba wamekubali kuuza kwa bei mpya iliyotangazwa na Ewura licha ya kulalamika kuwa ni bei ya hasara.

Alisema kampuni yake imekuwa ikipata hasara ya Sh117 kwa lita moja ya mafuta ya dizeli wakati hasara katika mafuta ya petroli ni Sh94.“Tumekubali agizo la Serikali siyo kutokana na amri yake pekee bali, hata sisi hatupendi nchi iingie kwenye matatizo. Tutaendelea kuuza kwa hasara hadi hapo tutakapofikia mwafaka,” alisema Bathawab.

Alisema pamoja na hatua hiyo bado wamiliki hao wanaendelea na mkutano na Ewura kujadili hatima ya sakata hilo.

BP yasuasua
Kwa upande wa Kampuni ya BP, jana walikuwa kwenye kikao kujadili agizo hilo la Serikali.Mwandishi wa gazeti hili alifika katika Ofisi za BP, Kurasini na kuelezwa kuwa viongozi walikuwa kikaoni na kwamba hakuna tamko ambalo lingetolewa mpaka kitakapomalizika.Mtumishi mmoja wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Agness Nsangalufu alisema: “Kwa sasa hivi hakuna taarifa yoyote kuna kikao kinaendelea labda nikupe namba ambayo ukipiga baadaye utapewa taarifa.”

Hata hivyo, namba hiyo ilipopigwa aliyepokea aliikata mara baada ya mwandishi kujitambulisha na haikupatikana tena hadi tunakwenda mitamboni.Mpaka saa 10 baadhi ya vituo kampuni hiyo vilikuwa havitoi huduma hiyo jambo lililoibua maswali mengi kutoka kwa wananchi hasa ikizingatiwa kwamba Serikali ina hisa katika kampuni hiyo.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Ewura, Titus Kaguo ilisema kampuni hiyo ilikuwa imetoa mafuta ya petroli lita 48,000 na dizeli lita 402,000 kwa ajili ya kuuzwa katika vituo vya rejareja.

Taomac yanywea
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kampuni za Kuuza Mafuta Tanzania (Taomac), Salum Bisarara alisema hawezi kuzungumzia kauli iliyotolewa na Serikali juzi kwa sababu ilielekezwa kwa kampuni.

“Serikali jana (juzi) ilielekeza kauli yake kwa kampuni za kuuza mafuta, kwa sasa suala lolote linalohusu bei ya mafuta sisi hatuwezi kulizungumzia, suala hili linatakiwa lizungumzwe na kampuni, sisi haturuhusiwi kupigania mambo ya bei za mafuta kabisa,” alisema na kuongeza:

“Ewura wametutahadharisha tusije tukavunja sheria kwa sababu suala hili limefika pabaya, hata suala la adhabu haturuhusiwi kulizungumzia.”

Mapema wiki hii Ewura iliweka bayana kwamba ingeishauri Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) kuifuta Taomac kutokana na kile ilichodai ni kukiuka sheria za biashara ya ushindani baada ya kukaa na kujadiliana kuhusu mgomo.

Wiki iliyopita, Bisarara alikaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba kutokana na bei elekezi iliyotolewa na Ewura, wafanyabishara wanapata hasara ya Sh150 mpaka 250 kwa kila lita hivyo kampuni hizo zitaweza kutoa huduma hiyo chini ya mwezi mmoja tu.

Ewura yatoa tamko
Kwa upande wake, Ewura imesema kuanzia jana, kampuni 13 ziliuza petroli na dizeli kwa ajili ya kusambazwa kwenye vituo vya rejareja.Taarifa ya Ewura imesema mbali ya BP, Kampuni ya Camel Oil ilitoa petroli lita 416,500 na dizeli 626,000, OilCom ilitoa petroli lita 353,000 na dizeli lita 382,000, Total ilitoa dizeli lita 163,000 na ORYX ilitoa petroli lita 44,000 na dizeli lita 91,000.

Kampuni ya Gulf Bulk ilitoa petroli lita 86,500 na dizeli 272,000, Engen ilitoa lita 64,000 za petroli na lita 175,000 za dizeli, MGS International ilitoa lita 116,000 za petroli.

Nat Oil ilitoa petroli lita 55,000 na dizeli 79,000. Lake Oil ilitoa lita 65,000 za petroli na dizeli lita 279,500. Gapco ilitoa petroli lita 418,100 na dizeli lita 348,500.

Kampuni ya Hass ilitoa petroli lita 119,000 na dizeli lita 57,500 wakati Kobil ilitoa lita za petroli 37,000 na lita 431,000 za dizeli.
 
(Habari hii ni kwa mujibu wa mtandao wa gazeti maarufu la Mwananchi)

 

Samsasali blogspot. Huyu jamaa ni noumer!

Kibogoyo Wake Mtori, Supu ataambulia Mchuzi.

Ni matumaini yangu ya kuwa wote tu wazima baada ya Long Weekend leo wengi tumerejea katika shughuli zetu za kile siku. Poleni na pilika pilika za Mafuta hapa mjini Dar-es-Salaam hali imekuwa tata, leo nimesikia watu wakiwalaumu EWURA kusababisha matatizo kwani wao walikuwa wananunua bei hiyo wanayotaka kimbelembele cha EWURA kujifanya inawajali wananchi kumbe ndo imewakera wananchi hahaha Tanzania ni Zaidi ya uijuavyo.

Ninakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Friends On Friday ya tarehe 5 August, 2011 haikuwa ya Kitoto Sifa na Utukufu tunamrudishia Mungu.

Katika utafiti wangu nimegundua watu wengi sana maarufu ama mashuhuri, umaarufu wao na umashuhuri wao uliwajia kama ajali, haikuwa katika moja wapo ya plan za maisha kufika pale walipofika, ndio maana wengi wao huwa hawadumu katika kile kilichowaweka juu, utakuta mtu ame struggle kufika sehemu fulani katika maisha ila akifika hapo juu anaanza kufanya mambo yanayommaliza yeye mwenyewe.

Shauku yangu nikiona watanzania hasa vijana kila Mtu aki simama kutimiza ndoto ya maisha yake, na nini unafanya kutimiza ndoto za wengine pia, mimi kama leo nimenyanyuliwa ninafanyaje kuwainua wengine. Wabongo wengi sisi ni vibogoyo inapofika swala la kutimiza ndoto zetu. Wengi tunapenda mambo mepesi mepesi hatupendi Big Stuff.

Kuna msemo ambao ni maarifu sana ulioongelewa naAliyekuwa Kiongozi wa Marekani Aleanor Roosevelt, aliwahi sema "Great Mind discuss about Ideas, Average Minds discuss Events and Small Minds Discuss People"

(Mengi zaidi yapo katika blogu yake... Jamaa ni creative nimependa sana.. We kamcheki halafu urudi uniambie umeonaje?)

Tembelea blog ifuatayo umcheki Missana Manyama na kazi ya mentoring: www.youthmentor.blogspot.com

YOUTH MENTOR: I CAN MOVE MOUNTAINS-2



If you simply believe you also can Move Mountains,Like Me; I do not mean the Physical Mountains, but the Mountains-in minds of the youth concerns:-
1. Social Mountains
2. Jobless Mountains
3. Economical Mountains
4. And the Like
Please your valuable comments are highly welcomed here under; suggest ways youth can go about -to solve these challenges/Mountains.


Haya na mengine mengi utayapata katika blogu hiyo...

Tuesday, August 9, 2011

Wenye Saluni Dar Walia na Mgawo wa Umeme

Wenye Saluni Dar Walia na Mgawo wa Umeme

WAFANYABIASHARA wa saluni jijini Dar es Salaam wamesema mgao wa umeme umewatia hasara kubwa na sasa wanafikiria kufunga biashara zao.

Wamesema mgao huo unasababisha hasara kwao kila siku kutokana na kutofungua saluni zao ambazo wanazilipia kiasi kikubwa cha fedha.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini kuwa saluni nyingi za kike na za kiume zimekuwa zikifungwa takribani siku nzima kutokana na mgao wa umeme katika maeneo mbalimbali jijini hapa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi, baadhi ya wamiliki wa saluni hizo katika maeneo ya Kimara, Sinza na Buguruni, walisema mgao wa umeme ni kikwazo kikubwa katika biashara yao.

Aisha Abdallah ambaye ni mmiliki wa saluni ya kike ya Baby Beauty saloon iliyopo Kimara Mwisho aliliambia Mwananchi kuwa tangu kuanza kwa mgao wa umeme, amekuwa akifanya kazi siku tatu tu kwa wiki, badala ya siku saba jambo ambalo alisema linanasababisha hasa kubwa kwake.

“Umeme unaniletea hasara kubwa sana, zamani nilikuwa nafanya kazi siku saba na kunifanya nipate fedha za kutosha kuendesha maisha yangu, kulipa kodi ya ofisi hii, lakini sasa hali naona inazidi kuwa mbaya kila kukicha, na mwenye kibanda anadai kodi yake kila mwezi, ni kero tupu” alisema Abdallah.

Alisema umeme katika maeneo hayo unakatika siku nne kuanzia asubuhi na kurudi usiku muda mbao hawezi kupata wateja na hivyo kumfanya ashinde siku nzima bila kuingiza pesa yeyote ile.

“Kawaida kwa siku nilikuwa nikipata Sh 30,000 katika siku za kawaida na Sh 50,000 kwa siku za mwisho wa wiki kiwango ambacho kiliweza kufikia malengo, lakini sasa mambo yameharibika maana nafanya kazi siku mbili au tatu kwa wiki na kufanya mapato yangu yaporomoke kwa zaidi ya asilimia 70”, alisema.


Bibi Harusi akiwa saluni. Shughuli nyingi zinazohusiana
na utengenezaji wa nywele hutegemea nishati ya umeme.

Naye Joel Sandi mmiliki wa saluni ya kiume ya Bon Love ya Sinza alisema kuwa mgao wa umeme umekuwa mwiba mchungu kwao na kwamba saluni zao zimekuwa ni kijiwe cha kupigia soga tu kutokana na kukosa umeme siku nzima.

“Kuna hatari ya kufunga biashara hii, maana uwezo wa kulipa kodi za pango haupo tena, na kama tutaendelea kufanya biashara hii itakuwa ni kwa ajili ya kulipia kodi tu, inakera sana na inabidi serikali ifanye mchakato wa kumaliza tatizo hili mapema,” alisema Sandi.

Alisema pamoja na kwamba baadhi saluni kubwa zinatumia jenereta wakati umeme ukikatika, lakini kwa wafanyabisahara wadogo hilo kwao ni gharama kubwa na kwamba hawawezi kulimudu.

Ni zaidi ya miezi miwili sasa tangu shirika la umeme nchini Tanesco
litangaze uwepo wa mgao wa umeme kwa nchi nzima jambo ambalo limeathiri sekta mbalimbali ikiwemo ya wajasiriamali kama hawa wa saluni.

(Habari hii ni kwa mujibu wa Gazeti Maarufu la Mwananchi)
Anthony Luvanda na kazi yake nzuri ya U-MC

Kwa wengine ni mara ya kwanza kulisikia jina hili. Kwa wengine jina hili si geni sana. Anthony Luvanda ni mtangazaji, mshereheshaji (MC), na mfanyakazi wa benki moja maarufu jijini Dar es Salaam. Hayo ni machache katika mengi usiyoyafahamu kuhusu kijana huyu mtanashati na aliyejaliwa vipaji lukuki na mwenyezi Mungu.

Kijana huyu ana majukumu mengi binafsi pamoja na majukumu mengine ya kijamii. Lakini leo ninataka kukudokeza kidogo tu kuhusu jukumu au kazi moja tu ambayo Anthony Luvanda amekuwa akiifanya kwa muda sasa na inayoonekana kumkaa kama vile alizaliwa nayo. Kazi hii si nyingine bali ni ya ushereheshaji, maarufu kama u-MC. Kwa lugha ya kiingereza ikijulikana zaidi kama ‘Master of Ceremony’.

Anthony Luvanda ambaye nimebahatika kusoma naye katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kufanya naye kazi katika sehemu mbili na nyakati mbili tofauti, kwa kweli ni mahiri sana katika kazi hii kiasi kwamba unaweza ukadhani amesomea mahali fulani.

Kutokana na umuhimu wa suala hili ambalo kwake ni kazi ama biashara, na kutokana na blog yangu kuwa inayohusu mambo ya shughuli za kibiashara, basi ni muhimu nikalielezea kwa marefu yake na mapana yake ili ninyi wasomaji wangu muweze kuelewa vizuri zaidi.

Hivyo basi kwa leo naomba niishie hapa, nikiwaacha na picha ya kijana huyu mahiri akiwa katika mojawapo ya shughuli zake katika moja ya matukio muhimu nchini.


 

Nitarejea kwenu muda si mrefu na mambo matamu na mazuri zaidi kuhusu shughuli hii na hususan kuhusu kijana huyu, Anthony Luvanda.

Asanteni sana.

Andrea Muhozya.

Blogu ya Mshauri wa Biashara Charles

 
Blogu ya Mshauri wa biashara Charles:
 
Charles P.M.Nazi ni Mshauri wa biashara anayejishughulisha na kutoa ushauri wa biahshara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa. Pia anatoa ushauri kwa wa uendeshaji wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO. Ana uzoefu katika kazi ya ukaguzi na uendeshaji wa asasi za kifedha SACCOS kwa miaka 20. Ametunga kitabu cha biashara kiitwacho Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Ofisi yake iko Sinza Kwa Remi katika majengo ya Princess Agnes Nursery School.Kwa mawasiliano piga simu namba 255755394701 au tuma barua pepe cnazi2002@yahoo.com
 

Malengo yake dira na mipango yake ya baadaye

MALENGO
Malengo yake ni kutoa huduma bora za ushauri kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,kwa SACCOS na Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.

DIRA
Anaamini kwamba matatizo yanayozuia maendeleo ya Wajasiriamali Tanzania ni pamoja na ukosefu wa mitaji na elimu ya biashara,hivyo lengo lake ni kuhakikisha anatoa elimu ya biashara na uendeshaji ili biashara na asasi ziweze kuendeshwa kwa ufanisi.
MALENGO YAKE
1.Kutoa ushauri wa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,
2.Kuandaa michanganuuo kwa ajili ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili..
3.Kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wafanyabiashara.
4.Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu na kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu..
5.Kuandaa katiba za vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni.
6.Kuandaa nyaraka za Tenda.
7.Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi.
8.Kutoa ushauri kwa Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
9.Kutunga vitabu za biashara ili kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi.
10.Kutoa ushauri nasaha na semina kwa wanafunzi.

MIPANGO YAKE YA BAADAYE
Kuimarisha biashara yake ili iweze kuenea mikoa yote ya Tanzania.

CHARLES P.M.NAZI
MSHAURI WA BIASHARA

Biashara Yako: Blogu Mpya kwa manufaa yako

Biashara-yako Blogspot!



Habari za wakati huu ndugu zangu.

Nawakaribisheni rasmi katika blog hii ya biashara-yako. Nimeanzisha blog hii kwa lengo maalum la kuzungumzia biashara mbali mbali zinazomilikiwa na watu wa kada mbali mbali hapa nchini Tanzania.

Lengo kuu ni kuonyesha ubunifu na uwezo tofauti katika kuendesha biashara; ili kutoa changamoto kwa wafanyabiashara wa sasa na wale wanaotarajia kufanya biashara baadaye.

Maoni, mawazo, na ushauri wenu vitazingatiwa sana katika kuifanya blog hii iwasaidie walengwa ambao ni sisi wenyewe na wenzetu pia.

Karibuni sana tushirikiane katika kuijenga nchi yetu.

Andrea Muhozya
Dar es Salaam
August 10, 2011