Wednesday, August 10, 2011

Tembelea blog ifuatayo umcheki Missana Manyama na kazi ya mentoring: www.youthmentor.blogspot.com

YOUTH MENTOR: I CAN MOVE MOUNTAINS-2



If you simply believe you also can Move Mountains,Like Me; I do not mean the Physical Mountains, but the Mountains-in minds of the youth concerns:-
1. Social Mountains
2. Jobless Mountains
3. Economical Mountains
4. And the Like
Please your valuable comments are highly welcomed here under; suggest ways youth can go about -to solve these challenges/Mountains.


Haya na mengine mengi utayapata katika blogu hiyo...

Tuesday, August 9, 2011

Wenye Saluni Dar Walia na Mgawo wa Umeme

Wenye Saluni Dar Walia na Mgawo wa Umeme

WAFANYABIASHARA wa saluni jijini Dar es Salaam wamesema mgao wa umeme umewatia hasara kubwa na sasa wanafikiria kufunga biashara zao.

Wamesema mgao huo unasababisha hasara kwao kila siku kutokana na kutofungua saluni zao ambazo wanazilipia kiasi kikubwa cha fedha.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini kuwa saluni nyingi za kike na za kiume zimekuwa zikifungwa takribani siku nzima kutokana na mgao wa umeme katika maeneo mbalimbali jijini hapa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi, baadhi ya wamiliki wa saluni hizo katika maeneo ya Kimara, Sinza na Buguruni, walisema mgao wa umeme ni kikwazo kikubwa katika biashara yao.

Aisha Abdallah ambaye ni mmiliki wa saluni ya kike ya Baby Beauty saloon iliyopo Kimara Mwisho aliliambia Mwananchi kuwa tangu kuanza kwa mgao wa umeme, amekuwa akifanya kazi siku tatu tu kwa wiki, badala ya siku saba jambo ambalo alisema linanasababisha hasa kubwa kwake.

“Umeme unaniletea hasara kubwa sana, zamani nilikuwa nafanya kazi siku saba na kunifanya nipate fedha za kutosha kuendesha maisha yangu, kulipa kodi ya ofisi hii, lakini sasa hali naona inazidi kuwa mbaya kila kukicha, na mwenye kibanda anadai kodi yake kila mwezi, ni kero tupu” alisema Abdallah.

Alisema umeme katika maeneo hayo unakatika siku nne kuanzia asubuhi na kurudi usiku muda mbao hawezi kupata wateja na hivyo kumfanya ashinde siku nzima bila kuingiza pesa yeyote ile.

“Kawaida kwa siku nilikuwa nikipata Sh 30,000 katika siku za kawaida na Sh 50,000 kwa siku za mwisho wa wiki kiwango ambacho kiliweza kufikia malengo, lakini sasa mambo yameharibika maana nafanya kazi siku mbili au tatu kwa wiki na kufanya mapato yangu yaporomoke kwa zaidi ya asilimia 70”, alisema.


Bibi Harusi akiwa saluni. Shughuli nyingi zinazohusiana
na utengenezaji wa nywele hutegemea nishati ya umeme.

Naye Joel Sandi mmiliki wa saluni ya kiume ya Bon Love ya Sinza alisema kuwa mgao wa umeme umekuwa mwiba mchungu kwao na kwamba saluni zao zimekuwa ni kijiwe cha kupigia soga tu kutokana na kukosa umeme siku nzima.

“Kuna hatari ya kufunga biashara hii, maana uwezo wa kulipa kodi za pango haupo tena, na kama tutaendelea kufanya biashara hii itakuwa ni kwa ajili ya kulipia kodi tu, inakera sana na inabidi serikali ifanye mchakato wa kumaliza tatizo hili mapema,” alisema Sandi.

Alisema pamoja na kwamba baadhi saluni kubwa zinatumia jenereta wakati umeme ukikatika, lakini kwa wafanyabisahara wadogo hilo kwao ni gharama kubwa na kwamba hawawezi kulimudu.

Ni zaidi ya miezi miwili sasa tangu shirika la umeme nchini Tanesco
litangaze uwepo wa mgao wa umeme kwa nchi nzima jambo ambalo limeathiri sekta mbalimbali ikiwemo ya wajasiriamali kama hawa wa saluni.

(Habari hii ni kwa mujibu wa Gazeti Maarufu la Mwananchi)
Anthony Luvanda na kazi yake nzuri ya U-MC

Kwa wengine ni mara ya kwanza kulisikia jina hili. Kwa wengine jina hili si geni sana. Anthony Luvanda ni mtangazaji, mshereheshaji (MC), na mfanyakazi wa benki moja maarufu jijini Dar es Salaam. Hayo ni machache katika mengi usiyoyafahamu kuhusu kijana huyu mtanashati na aliyejaliwa vipaji lukuki na mwenyezi Mungu.

Kijana huyu ana majukumu mengi binafsi pamoja na majukumu mengine ya kijamii. Lakini leo ninataka kukudokeza kidogo tu kuhusu jukumu au kazi moja tu ambayo Anthony Luvanda amekuwa akiifanya kwa muda sasa na inayoonekana kumkaa kama vile alizaliwa nayo. Kazi hii si nyingine bali ni ya ushereheshaji, maarufu kama u-MC. Kwa lugha ya kiingereza ikijulikana zaidi kama ‘Master of Ceremony’.

Anthony Luvanda ambaye nimebahatika kusoma naye katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kufanya naye kazi katika sehemu mbili na nyakati mbili tofauti, kwa kweli ni mahiri sana katika kazi hii kiasi kwamba unaweza ukadhani amesomea mahali fulani.

Kutokana na umuhimu wa suala hili ambalo kwake ni kazi ama biashara, na kutokana na blog yangu kuwa inayohusu mambo ya shughuli za kibiashara, basi ni muhimu nikalielezea kwa marefu yake na mapana yake ili ninyi wasomaji wangu muweze kuelewa vizuri zaidi.

Hivyo basi kwa leo naomba niishie hapa, nikiwaacha na picha ya kijana huyu mahiri akiwa katika mojawapo ya shughuli zake katika moja ya matukio muhimu nchini.


 

Nitarejea kwenu muda si mrefu na mambo matamu na mazuri zaidi kuhusu shughuli hii na hususan kuhusu kijana huyu, Anthony Luvanda.

Asanteni sana.

Andrea Muhozya.

Blogu ya Mshauri wa Biashara Charles

 
Blogu ya Mshauri wa biashara Charles:
 
Charles P.M.Nazi ni Mshauri wa biashara anayejishughulisha na kutoa ushauri wa biahshara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa. Pia anatoa ushauri kwa wa uendeshaji wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO. Ana uzoefu katika kazi ya ukaguzi na uendeshaji wa asasi za kifedha SACCOS kwa miaka 20. Ametunga kitabu cha biashara kiitwacho Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Ofisi yake iko Sinza Kwa Remi katika majengo ya Princess Agnes Nursery School.Kwa mawasiliano piga simu namba 255755394701 au tuma barua pepe cnazi2002@yahoo.com
 

Malengo yake dira na mipango yake ya baadaye

MALENGO
Malengo yake ni kutoa huduma bora za ushauri kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,kwa SACCOS na Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.

DIRA
Anaamini kwamba matatizo yanayozuia maendeleo ya Wajasiriamali Tanzania ni pamoja na ukosefu wa mitaji na elimu ya biashara,hivyo lengo lake ni kuhakikisha anatoa elimu ya biashara na uendeshaji ili biashara na asasi ziweze kuendeshwa kwa ufanisi.
MALENGO YAKE
1.Kutoa ushauri wa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,
2.Kuandaa michanganuuo kwa ajili ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili..
3.Kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wafanyabiashara.
4.Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu na kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu..
5.Kuandaa katiba za vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni.
6.Kuandaa nyaraka za Tenda.
7.Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi.
8.Kutoa ushauri kwa Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
9.Kutunga vitabu za biashara ili kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi.
10.Kutoa ushauri nasaha na semina kwa wanafunzi.

MIPANGO YAKE YA BAADAYE
Kuimarisha biashara yake ili iweze kuenea mikoa yote ya Tanzania.

CHARLES P.M.NAZI
MSHAURI WA BIASHARA

Biashara Yako: Blogu Mpya kwa manufaa yako

Biashara-yako Blogspot!



Habari za wakati huu ndugu zangu.

Nawakaribisheni rasmi katika blog hii ya biashara-yako. Nimeanzisha blog hii kwa lengo maalum la kuzungumzia biashara mbali mbali zinazomilikiwa na watu wa kada mbali mbali hapa nchini Tanzania.

Lengo kuu ni kuonyesha ubunifu na uwezo tofauti katika kuendesha biashara; ili kutoa changamoto kwa wafanyabiashara wa sasa na wale wanaotarajia kufanya biashara baadaye.

Maoni, mawazo, na ushauri wenu vitazingatiwa sana katika kuifanya blog hii iwasaidie walengwa ambao ni sisi wenyewe na wenzetu pia.

Karibuni sana tushirikiane katika kuijenga nchi yetu.

Andrea Muhozya
Dar es Salaam
August 10, 2011